Moja kati ya mambo yanayo suasua katika kuifanya East Africa community kukua zaidi ni suala la biashara na mifumo ya kikodi. Mpaka hivi sasa nchi washirika zinaendelea kuumiza vichwa kukubaliana mfumo utaofaa kutumika ambao utatoa usawa katika kufaidisha pande zote husika katika biashara zinazovuka mipaka.
Lakini hayo yakiendelea kufanyiwa vipimo, Watupipo tumefanya observation na kugundua kua kwa kua michezo na sanaa ni sekta ambazo zikipewa umakini wa hali ya juu zinaweza kusaidia kuiunganisha Africa mashariki zaidi hasa na kutoa fursa nyingi za ajira zaidi ya zile zinazopatikana sasa.
Katika shughuli zetu za michezo zinazofanyika mkoani Mara, tumeona vile ambavyo raia kutoka Kenya wanafika na kuendelea na shughuli za michezo na biashara katika kijiji cha Nyamongo bila kupata aina yoyote ya changamoto kutoka kwa wenyeji.
Kwa kuliona hili Watupipo kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo na burudani tunakuja na mpango wa kuzalisha ajira na kuwakutanisha vijana wa Africa Mashariki kupitia soka na muziki mwaka 2024.